| Wanajeshi hao wa jeshi la nchi ya NEPAL wakiwa wanaonyesha vyeti vyao vya uanajeshi wa jeshi hili |
Idara
ya uhamiaji Jijini Dare s salaam imewakamata raia 12 wa kigeni
waliokuja nchi kinyume na sheria wakiwemo wanajeshi wanne wa jeshi
la NEPAL pamoja na nane kutoka nchini india walioletwa nchini kinyume
na sheria kwa kisingizio cha maisha magumu nchini kwao.
Raia hao
wamekamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya ESCOT iliyoko kijitonyama
jijini Dar es salaam katika operation maalum iliyoendeshwa na idara ya
uhamiaji Jijini baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi wa maeneo
hayo juu ya uwepo wa watu hao ambao waliwatilia mashaka.
| Afisa uhamiaji wa jiji la Dar es salaam GRACE HOKORORO akizungumza na mtandao huu kuhusu sakata hilo |
Wanajeshi
hao wanne wa jeshi la NEPAL yumo pia komando mmoja wa jeshi hilo ambao
nao wamedai kuletwa nchini kwa ajili ya kutafutiwa ajira ya maswala ya
ulinzi katika nchi za Africa hivyo wakashukia Tanzania kama kituo kwa
ajili ya kufanikisha malengo yao.
Akizungumza na mtandao huu muda mfupi uliopita afisa wa uhamiaji
wa jiji la Dar es salaam GRACE HOKORORO amesema kuwa wahamiaji hao
wamekuwa wakipita katika nchi ya Tanzania na kupelekea nchi nyingine
kama Africa ya kusini kwa ajili ya kufanyishwa kazi zisizo halali
| Picha mbili zikionyesha wanajeshi hao wakiwa katika nchi yao wakiwa wanalitumikia jeshi la nchi yao kabla ya kutimka na kuja nchini |
Aidha amesema kuwa watu hao wamekuwa wakiletwa na mawakala ambao
wamekuwa wakiwatoa katika nchi zao kwa ahadi la kuwatafutia kazi katika
nchi hizi jambo ambalo amesema kuwa linatafsiriwa kama biashara ya
binadamu ambapo mawakala waliowaleta watu hao hadi sasa hawajapatikana.
Aidha Bi GRACE amewataka watanzania na watu wasamaria wema
kuwafichia watu wanaowaficha watu kama hao kwani ni kinyume na sheria na
baadae huleta madhara makubwa kama uhalifu na uuzwaji wa madawa ya
kulevya.