Katika Hali Isiyo ya Kawaida Wafanyakazi wa NSSF Mkoa wa Njombe Wamejikuta Wakilikimbia Jengo Lao Baada ya Kifaa Kilichofungwa Kwa ajili ya Kutoa Tahadhari ya Hatari Kupiga Alam Kuashiria Kuna Tatizo Linaloweza Kutokea.
Taharuki Hiyo Imetokea Leo Majira ya Saa Nne Asubuhi na Kusababisha Kazi Kusimama Kwa Takribani Saa zima na Kuwasababishia Usumbufu Wateja wa Mfuko Huo wa Hifadhi ya Jamii.
Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Katika Eneo la Tukio Afisa wa Polisi wa Kikosi Cha Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Njombe Coplo Rashid Cassim Amesema Kuwa Kama Zima Moto Wamepewa Taarifa ya Tukio Hilo na Kisha Kufika Kuangalia Tatizo Hilo Ambapo Wamebaini Kuwepo Kwa Hitilafu ya Kifaa Hicho Ambacho Wamelazimika Kukata Nyaya zake Kutokana na Kutokuwa na Namba za Siri.
Amesema Kuwa tatizo hilo hutokea mara Chache katika maeneo tofauti hususani pale wanakuwa wanataka kujaribu kama kifaa hicho kinafanya kazi ambapo pia hutoa taarifa na kwamba tatizo lololeta kama vumbi inaponasa katika kifaa hicho huleta shorti na Alam ya hatari.
Gowin Mwakalukwa ni Meneja wa Mfuko wa NSSF Mkoa wa Njombe Ambaye Amesema Kuwa Hadi sasa kinachoendelea ni Kufanya mawasiliano na watu waliofunga kifaa hicho ili waje kuweka namba za siri[pass word]katika kifaa hicho ili waruhusu kiendelee kufanya kazi.
Katika Hatua Nyingine Bwana Mwakalukwa Amewataka wafanyakazi na wateja wote wanaofika katika ofisi hizo kuacha kuvuta sigara kwani imeelezwa kuwa kifaa hicho huleta shida endapo harufu ya sigara inatokea.
Hata hivyo amewaomba radhi wateja wote waliofika kupata huduma ofisini hapo na kukutana na hali hiyo.