MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA TABORA AJIUZULU RASMI, ADAI KATIBA INAKIUKWA NA VIONGOZI WA JUU.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoa wa Tabora Bw.Kansa Mbaruku na Mwenyekiti wa kamati ya Sheria na haki za binadamu kanda ya magharibi ambaye pia ni Mwanasheria mkongwe Bw.Mussa Kwikima wametangaza kujiuzulu rasmi leo hii mbele ya waandishi wa habari kufuatia madai ya kuendelea kukiukwa kwa maadili ya viongozi kuanzia ngazi ya juu ambao wamekuwa wakivunja katiba kwa maslahi yao binafsi.

Kujivua madaraka kwa viongozi hao wawili huenda ikawa pigo kubwa kwa Chadema kanda ya Magharibi baada ya mmoja kati ya makada mahili wa chama hicho wilaya ya Igunga Bw.Anuar Kashaga kuondoka Chadema na kujiunga na Chama cha Mapinduzi katika siku za hivi karibuni.

Hatua ya  kuachia ngazi kwa viongozi hao imedaiwa kuwa kuna siri nzito ya wimbi la ubaguzi wa kikabila,kikanda na hata kidini ambayo bado viongozi hao wamekuwa na kigugumizi kuweka hadharani.

NA KAPIPI J


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo