MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU ABAKWA, ATOBOLEWA MACHO NA KUUAWA.

Mtoto mwenye umri wa miaka 9 (Jina tunalihifadhi) mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Negezi iliyopo kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga ameuawa kikatili kwa kubakwa kisha kutobolewa macho na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa kichakani.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana saa saba mchana katika kitongoji cha Kashampa kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi ambapo mwili wa marehemu ulikutwa kichakani.

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Dkt Daniel Maguja amesema vipimo vinaonesha kuwa mtoto huyo alibakwa na kutobolewa macho.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo  na kuongeza kuwa chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa huku akitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kuwabaini na kuwakamata wauaji ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Na Kadama Malunde-Shinyanga


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo