Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe mwenye shati la Kitenge wa pili
kushoto akitoa maagizo kwa msisitizo huku akionesha ishara ya mikono
kwa Mamlaka ya Maji Mjini kuhakikisha wanalinda na kuhifadhi chanzo cha
maji cha Mto Ikolongo wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa Bodi ya
Mamlaka ya Maji Mjini Mpanda Mama Anna Lupembe Mwenye Tishirt nyeupe
pamoja na viongozi wengine wa Halmashauri ya Mji Mpanda.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maji safi na taka wa Mji wa Mpanda Mhandisi Zacharia
Nyanda mwenye shati nyeupe na anayenyosha mkono kuonesha eneo la chanzo
wakati akitoa maelezo mafupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi wa Katavi Dkt
Rutengwe anayemsikiliza kwa umakini kuhusu chanzo cha maji cha Mto
Ikolongo akimweleza kuwa eneo hilo ndio mradi wa Maji ya Mseleleko
yanayotumiwa na wakazi wa Mjini
Wakazi
wa Ikolongo makazi ya Wakimbizi Katumba wakitoka kuchota maji kwenye
chanzo cha maji ya mto huo kama walivyokutwa na mpiga picha wetu.
…………………………………………………………………………………………..
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe,ameiagiza Mamlaka ya Maji Mjini Mpanda kwa kushirikiana na Idara ya Maji pamoja na Idara
ya Mazingira kulinda na kuhifadhi chanzo cha maji cha Mto Ikolongo
ambacho ni tengemeo kubwa kwa Mseleleko yanayotumiwa na Wakazi wa Mji
wa Mpanda.
Dkt
Rutengwe alitoa agizo hilo muda mfupi baada ya kutembelea chanzo hicho
na kujionea hali halisi katika mto huo ulioko umbali wa takribaini
kilometa 24 kutoka Mjini Mpanda .
Mbali
ya kuhifadhiwa pia ameagiza kupanda miti kuzunguuka chanzo hicho
kilichopo eneo la Ikolongo Makazi ya Wakimbizi Katumba.
Pamoja
na kuhimiza kulinda chanzo hicho pia ameutaka uongozi wa Mamlaka ya
Maji safi na taka katika Mji wa Mpanda kwa kushirikiana na Uongozi wa
Halmashauri kuona namna ya kuwatengenezea miundombinu ya maji wakazi
wanaoishi jirani na chanzo vyanzo vya maji ili waweze kuwa na moyo wa
kuvilinda.
Iwapo
watapatiwa huduma ya maji itakuwa rahisi kwao kwa kuwa na moyo na
ari ya kuendelea kulinda na wala hawawezi kuharibu mazingira ya vyanzo
vya maji kwa kuwa wanafahamu umuhimu na manufaa yake kwao.
Iwapo
watatengenezewa mabomba na kuwekewa maji ya bomba yanayotoka katika
chanzo wanachohifadhi watakuwa waelewa na watanufaika na wenyewe kuliko
kuwaacha kama walivyo
Akaongeza
kuwa iwapo watatumia maji ya kwenye chanzo inachangia kwa njia moja au
nyingine kuharibu mazingira pamoja na uchafuzi zaidi kwa kuwa maji hayo
yanatengemewa na watu wengi kwa maisha yao.
“Hakikisheni
wananchi hao wanaoishi jirani na chanzo hiki wanapata maji ili
wasiendelee kuharibu chanzo hiki wasiendelee kufulia na kunyweshea
mifugo yao katika chanzo hiki kilindwe na kutunzwa,iwapo mtafanya hivyo
mtakuwa mmesaidia sana kuoko chanzo hiki.”alisema Dkt Rutengwe.
Akiongelea
namna ya kuweza kupaendeleza na kupahifadhi ili kuweze kuwapa umuhimu
zaidi,ameeleza kuwa chanzo hiki ni utajiri mkubwa na huenda ikawa Mkoa
wa kwanza wenye chanzo cha maji kizuri kilichohifadhi na kutunzwa vizuri
hivyo haina budi kuendelea kukilinda na kukihifadhi kwa gharama yeyote
huu ni utajiri wa kipekee,huwezi kuwa masikini ukiwa na chanzo kizuri
namna hiyo alieleza Mkuu wa Mkoa huyo.
Akizungumzia
kuwazuia wananchi kutumia eneo hilo kwa shughuli za kibinadamu kama
kuchota maji,kufua na shughuli nyingine alieleza kuwa huwezi kumzuia
mwananchi akakuelewa bila kuweka utaratibu mzuri wa namna atakavyoweza
kuendelea kupata huduma aliyokuwa akiipata.
“Haiwezekani
kumkataza mwananchi kuchota maji katika eneo hili wakati hujamwandalia
mazingira mazuri mbadala ya yeye kupata huduma ya maji,hilo halikubaliki
watengenezeeni haraka sana mazingira ya wao kupata huduma ya maji kisha
ndio muweke utaratibu mzuri wa kuwakataza wasitumie kuja kuchota maji,
wala kutumia eneo hili kwa shughuli za kibinadamu kwa kuwa shughuli za
kibinadamu zitaharibu chanzo hiki”alisema Mkuu wa Mkoa kwa Msisitizo.
Awali
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Anna Lupembe alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa
eneo hili ni hazina kwao na wameweka mpango mzuri wa kuliombea fedha
kutoka wizarani ili kuliendeleza na kuwapatia maji safi wananchi wa
Mpanda na Mkoa kwa ujumla.
Mwenyekiti
huyo alieleza kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mhandisi Zacharia
Nyanda alipofika tu katika Mkoa huo Halmashauri ya Mji wa Mpanda
alitengeneza maandiko ya kuomba fedha kwa ajili ya kuweza kuendeleza
chanzo hiki ili kiweze kuwanufaisha wananchi wa Mpanda waweze kupata
maji safi.
Alisema
kutokana na Andiko lililoandikwa kuomba fedha zimepatikana karibu
shilingi bilioni tatu ambazo ziatasaidia kusambaza maji katika mji wote
wa mpanda na maeneo ya jirani kwenye vijiji vinavyozunguuka Mji huo,
ameyataja maeneo yaliyoko nje ya mji ambayo yanaweza kunufaika na mradi
huu wa maji kutoka chanzo cha maji mto Ikolongo kuwa Vijiji vilivyoko
Kata ya Magamba Halmashauri ya Nsimbo,Mtapenda,Kasokola Nsimbo
yenyewe,Milala,na Kakese.