Kitengo cha sheria nchini ya Marekani kimeanza kufanya uchunguzi wa jinai dhidi ya kifo chamwandishi wa habari mwenye asili ya Marekani ,James Foley aliyeuawa na wapiganaji wa kiislamu wenye msimamo mkali.
Mwanasheria mkuu wa kitengo hicho,Eric Holder
ameweka wazi kuwa wote waliohusika na mauaji ya mwandishi huo watawatia
mkononi muda si mrefu.
Maofisa wa serikali ya Marekani wanadai kwamba
askari hao wauaji walidai kiasi kikubwa cha pesa zipatazo dola za
kimarekani zaidi ya milioni mia moja na thelathini kama fidia ya
kumuachilia James Foley.
Marekani imekwisha anza harakati za kuwasaka na
hatimaye kuwakamata waliohusika na mauaji ya mwandishi huyo kwa kurusha
ndege zake takriban sita katika anga inayomilikiwa na waislamu kaskazini
mwa Iraq.
