Habari ya Mjini ni kuhusu Jokate Mwegelo kutoka kimapenzi na Ommy Dimpoz ambaye ni star wa Bongofleva.
Habari zaidi zinasema kuwa Jokate na Ommy Dimpoz
wamekuwa wapenzi kwa muda sasa ila kwa siri kubwa ikidaiwa wote hawakuwa
tayari kuweka uhusiano wao hadharani wakiogopa media kuanza kuwafuatilia.
Inadaiwa pia kuwa Ommy alikuwa anatoka kimapenzi na Vanessa Mdee lakini
baada ya Vanesa kugundua kuwa Jokate anamzunguka zikawa haziivi tena na
huchekeana kinafiki tu wakikutana .
Kwasasa Jokate na Ommy
wanaliendeleza libeneke la huba kwa siri.Habari zinaingia ndani zaidi kwa kusema kuwa Jokate
alikuwa pia akienda mikocheni alipodaiwa alikuwa nakaa Dimpoz sababu ya
penzi kukolea.
Hata hivyo si Jokate, Ommy wala Vanessa ambaye amepatikana kuzungumzia suala hili

