Rapper wa Young Money, Nicki Minaj aliachia video ya ‘Anaconda’ ambayo kimaadili bila kusita haifai na huenda wengi bado tunasubiri kuona video nyingine ya toleo safi.
Kwa bahati mbaya hakutakuwa na toleo safi la video hiyo ambayo kila sekunde yake ina mengi.
Akiongea na Nick Martinez katika mahojiano maalum kabla ya kuachia
rasmi video hiyo, rapper huyo ameeleza kuwa hajui ni jinsi gani anaweza
kufanya toleo safi la video ya wimbo huo.
“Nilikuwa nasema tangu awali kuwa sijui ni jinsi
gani ntakuja kufanya clean version (safi kimaadili) ya hii video.”
Amesema Nicki Minaj.
Rapper huyo pia alizungumzia ujumbe aliolenga kuufikisha kwa wasichana wenzake kama msanii kupitia video hiyo.
“Moja kati ya vitu ambavyo nilitaka kufanya na huu wimbo ilikuwa
kupeleka ujumbe kwamba kuwa na makalio makubwa au madogo (sio
tatizo)….najua kwa sababu mimi niko kwenye biashara, niko kwenye
pressure ya kuwa mwembamba sana, unajua kwa kweli nataka kupungua uzito
hata sasa hivi.
“Lakini sitaki kutuma ujumbe kwa wasichana wengine kuwa sio kila
wakati wanapoangalia kwenye TV wataona mtu wa ‘kijamii’ kwa sasabu sio
uhalisia.” Alieleza.
Ameongeza kuwa aliamua kutoa ‘cover’ ya aina ile ikionesha makalio
makubwa kwa sababu huona models ambao ni wembamba sana na huonesha
makalio yao mara nyingi lakini haionekani kama ni kitu cha ajabu.
Kama hukuiona, Itazame hapo chini
Kama hukuiona, Itazame hapo chini
