WAENDESHA BODABODA WAOMBA MAMLAKA HUSIKA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA WEZI WA PIKIPIKI

Waendesha pikipiki za kubeba abiria maarufu kama boda boda, wamezitaka mamlaka za kisheria kuwachukulia hatua kali watuhumiwa wanaobainika kujihusisha na wizi wa pikipiki, ambao wamedaiwa kurudisha nyuma jitihada zao za kujikwamua na umaskini, badala ya kuwakamata na kuwaachia,jambo linalowafanya wengi wao kuamua kujichukulia sheria mikononi kwa kuwaadhibu.
 
Waendesha pikipiki hao wamesema hayo walipohojiwa  kuhusiana na wenzao kujichukulia sheria mikononi kwa kumpiga hadi kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, mtuhumiwa Shafii Shomari, aliyedaiwa kushirikiana na mwenzake  kumpora pikipiki Saidi Omari,baada ya kumkodi kutokea eneo la Itigi Msamvu, wakitaka kupelekwa eneo la Mapumbani,kabla ya siku chache baadaye pikipiki hiyo kukutwa nje ya nyumba ya mwenyekiti wa mtaa wa Mwembesongo,Nasoro Samata,aliyedai kuachiwa  pikipiki hiyo kama dhamana na mtu aliyechukua kwake mkopo wa shilingi 50,000. 
 
Akizungumzia tukio hilo la wizi wa pikipiki, kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro  Leonard Paulo, amewashuruku raia wema waliofanikisha kupatikana kwake baada ya kuibwa, na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi wa tukio hilo ikiwemo kumhoji mwenyekiti huyo wa mtaa na kuchunguza namna alivyoipata pikipiki hiyo
 
>>>itv


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo