MWILI WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KINYAMA KWA WIVU WA KIMAPENZI WAOKOTWA MKOANI LINDI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga.
 
MWILI wa mwanamke mwingine aliyetambulika kwa jina la Zuhura Mtenda mwenye umri wa miaka, 32 umeokotwa leo na kufanya idadi ya wanawake waliouawa mpaka sasa katika Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kufikia nane.

Wanawake hao nane waliouawa kikatili mpaka sasa wana umri kati ya miaka 18-32.

Chanzo cha mauaji hayo kimedaiwa kuwa ni uhusiano wa kimapenzi.

Katika kuonyesha kuwa wamekerwa na vitendo hivyo, baadhi ya wananchi wilayani humo, leo wamezingira Kituo Kikuu cha Polisi Nachingwea, kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nne wakitaka polisi kuwaruhusu kuwa waue watuhumiwa watatu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo ambapo polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga, amesema wananchi hao wenye hasira walikuwa wamezunguka kituo hicho cha polisi wakitaka kuwaua watuhumiwa watatu wanaoshukiwa kuwa ndio wahusika wa baadhi ya mauaji ya wanawake hao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo