Mastaa wa filamu nchini Diana Kimaro na Manaiki Sanga ni
wapenzi. Juzi zilipenyezewa habari kuwa Manaiki anatoka na Diana
Kimaro na kwasasa wameshibana vya kutosha kila mtu yupo hoi kwa mwenzake
kama mlenda.
Uzuri ni kuwa wakati udaku huo ukipenyezwa
Manaiki mwenyewe alikuwepo eneo hilo
ambapo wasanii kadhaa walikuwa wakifuturu pamoja hivyo haraka sana
tukampiga swali la moto Manaiki kama ni kweli yeye na Diana kwasasa ni
honey, sweet na mpenzi?
Manaiki alibaki kuangua kicheko ambacho kilitoa
jibu la moja kwa moja kuwa hajiwezi kwa Diana ambaye kadri siku
zinavyozidi kwenda ndivyo anavyozidi kujiimarisha kwenye tasnia ya
filamu Swahiliwood.
Pia kupitia mitandao ya kijamii Manaiki amekuwa akiandika ujumbe na kupost picha akiwa na Diana. moja wa ujumbe huo ni huu:
"#love #never #die japokua haupo na Mimi ila everyday mi naku feel baby sijuwi kupendwa kama we ulivyokua unanipenda na hiyo ni habari ya mjini"
"#love #never #die japokua haupo na Mimi ila everyday mi naku feel baby sijuwi kupendwa kama we ulivyokua unanipenda na hiyo ni habari ya mjini"

