MTOTO AFARIKI DUNIA AKIOGELEA KWENYE DIMBWI LA MAJI

WATU wawili akiwemo mtoto Ayubu Hassan anayekadiriwa kuwa na miaka 7-10, mkazi wa Tungi Mnadani, Kigamboni jijini Dar es Salaam wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti.

Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alisema mtoto huyo alifariki juzi baada ya kutumbukia kwenye dimbwi la maji majira ya saa 5 asubuhi.

Kiondo alisema kuwa maiti ya mtoto huyo mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kisiwani, ilikutwa ndani ya dimbwi hilo lililochimbwa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Shirika la Umeme (Tanesco).

Alisema kwamba taarifa za awali zinaonyesha mtoto huyo alikuwa akiogelea na wenzake na ndipo alipozama kwenye maji, hatimaye kufariki na maiti yake kuhifadhiwa Hospitali ya Vijibweni.

Katika tukio jingine, mfanyabiashara mkazi wa Keko, aliyetambulika kwa jina moja la Chuka (40), amefariki dunia baada ya kugongwa na gari la Kampuni ya Express.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 10:11 asubuhi barabara ya Kawawa eneo la Kigogo Sambusa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo