Mrembo Doreen aliyekuwa video Queen wa wimbo uliotokea kutamba miaka ya nyuma wa Ice Cream ulioimbwa na Haji Nura 'Noorah' akimshirikisha Suma Lee ameanza kurejea katika hali yake ya kaaida ikiwa ni baada ya kutopea katika matumizi ya dawa za kulevya.....
Doreen
anakuwa wa kwanza kuionyesha jamii juu ya taasisi ya
mwanamuziki Rehema Chamila 'Ray C' ya Ray C Foundation kuanza
kutimiza malengo yake baada ya kufanikisha mrembo huyo kuanza
kutumia tiba ya dawa za Methadone na afya yake kuanza kurejea
kwenye hali yake ya kawaida.....
Ray C akizungumza na mwandishi wetu amesema kuwa anajisikia fahari kuona afya ya Doreen ikiimarika kwa haraka.
"Karudi
katika hali yake ya kawaida baada ya kuanza tiba ya
Methadone......Nafurah sana nikiona matuda ya Ray C Foundation,
nimefurahi kumuona akiwa na afya njema," amesema Ray C.
Ray
C ni mwanamuziki wa kwanza nchini kujitoa mhanga kuwasaidia
vijana waliojiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya