MBUNGE ATAKA ARUSHA IWE KANDA MAALUM YA KIPOLISI, KISA MABOMU

Mbunge wa viti maaluma Arusha Catherine Magege ameiomba serikali kuanzisha kanda maalumu ya kipolisi kwa jiji la Arusha ili kuimarisha ulinzi ambao umekuwa ukizorota siku hadi siku huku maisha wa wakazi wake yakiwa hatarini.

Kufuatia mfululizo wa mabomu baadhi wa kazi wa jiji la Arusha wameiomba serikali kuingilia kati swala hilo kwa kuwa watu wamekuwa na hofu ya kushiriki katika matukio mbalimbali hasa yale ya mikusanyiko ya watu kwa kuhofia milipuko.
 
Hata hivyo Jeshi la Polisi nchini Tanzania linawashikilia watu wawili kuhusiana na mlipuko uliotokea katika Mgahawa wa Vama Traditional Indian Culture uliopo karibu na viwanja vya Gymkhana na Mahakama Kuu Jijini Arusha.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo