Mmoja wa wanajeshi wa Boko Haram ambaye hakutaka
kujitambulisha jina alizungumza na BBC jana (July 8) na kueleza hali na
afya ya wasichana zaidi ya 200 wanaoshikiliwa na kundi hilo, taarifa
ambazo zilikuwa tofauti na zile za awali zilizokuwa zikitolewa na
maafisa wa Nigeria.
Mtu huyo alisema kuwa wasichana hao wako katika hali salama na wana
afya njema tofauti na ripoti alizozitoa Senator kuwa walikuwa wakibakwa
wakichukuliwa video na wengine wakiuawa endapo wangekaidi.
Hata hivyo mtu huyo aliweka wazi msimamo wa kundi hilo kuwa
watawaachia wasichana hao siku moja baada ya serikali ya Nigeria
kuwaachia wafungwa wa kundi hilo wanaowashikilia.
Hivi ndivyo alivyoeleza:
“Kweli tunataka serikali ya Nigeria kuwaachia watu wetu. Kama
kiongozi wetu Abubakar Shekau alivyoahidi kwenye vyombo vya habari, kama
leo serikali itaawaachia watu wetu, kesho au siku inayofuata tunaahidi
mtawaona wasichana wote. Tutaweza kuwaachia kesho ama siku inayofuata.
Ninawaambia ukweli, wako katika hali nzuri wakisubiri kuachiliwa. Hawana
tatizo. Baadhi wamebadili dini na kuwa waislam, wengine hawakubadili
dini lakini hatukuwatofautisha, tunawatunza kwa usawa...”
