Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha |
Matukio
ya mauaji ya wanawake vikongwe kutokana na ugomvi wa mashamba
yameendelea kujitokeza mkoani Shinyanga ambapo huko katika kitongoji na
kijiji cha Magwata kata ya Mwamalili katika manispaa ya
Shinyanga,mwanamke aitwaye Sayi Nyenje(75) ameuawa kwa kukatwa mapanga
shingoni na kiganjani akiwa amelala na wajukuu zake.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka wa kamanda wa polisi
mkoa wa Shinyanga SAP Justus Kamugisha tukio hilo limetokea Julai
23,mwaka huu saa 11 alfajiri.
Kamanda
Kamugisha alisema mwanamke huyo Sayi Nyenje(75) mkazi wa Mwamalili
katika manispaa ya Shinyanga akiwa nyumbani kwake amelala na wajukuu
zake wawili alivamiwa na watu wawili wanaume kisha kumkata panga
shingoni na kiganja cha mkono wa kushoto na kusababisha kifo chake papo
hapo.
Tayari
jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa mmoja aitwaye Joel Machia(45)
mkazi wa Mwamalili na mwenzake ametorokea kusikojulikana.
Alisema
chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa lakini kuna tetesi za uwepo
wa ugomvi wa mashamba kati ya marehemu na mtuhumiwa aliyekamatwa.
Aidha
alisema jeshi la polisi linaendelea na juhudi za kumtafuta mtuhumiwa
mwingine huku akiwataka wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa
kwa mtuhumiwa huyo.
Tukio la mauaji ya kikongwe huyu limetokea ikiwa hata wiki mbili hazijaisha baada yamwanamke
aitwaye Milembe Masanja(50) mkazi wa kitongoji cha Muhida kijiji na
kata ya Busangi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kuauawa kikatili kwa
kukatwa panga kichwani na mikono yote na watu wawili walikodishwa
kutekeleza mauaji hayo.
Tukio hilo limetokea Julai 14 mwaka huu saa mbili usiku.
Ambapo
Milembe Masanja aliuawa kwa kukatwa panga kichwani na mikono yote
miwili na watu wawili ambao ni Chuchu Lugodisha na mwenzake Ngeja
Kugodisha wote wakazi wa kijiji cha Izumba kata ya Luguya mkoani Tabora.
Kwa
mujibu wa kamanda Kamugisha watu hao walikodiwa na Madaha Luhemeja ili
kufanya mauaji hayo ambapo ilielezwa kuwa familia ya marehemu ilikuwa na
ugomvi wa mipaka ya mashamba na familia ya Madaha Luhemeja.
Na Kadama Malunde-Shinyanga