"HOUSE GIRL" WA MFANYAKAZI WA BENKI AUAWA KWA KUNYONGWA CHUMBANI KWAKE SHINYANGA

Matukio ya mauaji yameendelea kuukumba mkoa wa Shinyanga ambapo huko katika mtaa wa Majengo Mapya Mjini Shinyanga, mfanyakazi wa ndani, Eliwaza Damiano (15)  ameuawa kwa kunyongwa kwa kutumia nguo aina ya khanga katika chumba chake cha kulala katika nyumba ya muajiri wake.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa moja usiku ambapo mfanyakazi huyo wa ndani wa alikutwa ameuawa  kwa kunyongwa na watu wasiojulikana ambao pia waliiba kompyuta mpakato(Laptop) moja,mkoba wa mkononi ukiwa na shilingi 20,000/= kisha kutokomea kusikojulikana.

Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo,na kamanda wa polisi Justus Kamugisha amesema mwili wa marehemu uligunduliwa na muajiri wake Elizabeth Joseph (38) ambaye ni mfanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Shinyanga mjini ambaye baada ya kutoka kazini alimkuta mfanyakazi wake ameuawa.

Kamanda Kamugisha ameongeza kuwa katika uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa marehemu aliuawa kwa kunyongwa na khanga shingoni na watu wasiojulikana.

Na Kadama Malunde-Malunde1 blog-Shinyanga


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo