Kama ulikuwa Hewani siku ya jana katika kipindi maarufu kabisa (XXL),
ndani ya Stetion maarufu hapa Tz yaani nazungumzia CLOUDS Fm utaelewa
nini ninachozungumzia mpaka sasa.
Katika hali isiyotegemewa jana watangazaji watatu maarufu kama, DJ
FETTY, ADAM MCHOVU na B12 waliziweka ndani ya studio za Clouds live huku
wakisahau kuwa Wasikilizaji wanawasikia mwanzo mwisho wanachokifanya
huko ndani ya studio. Sakata hilo limesababisha na kutoelewana baina ya
hawa watangazaji juu ya mauzo ya Albam ya Fiesta!
Sasa leo watu mbalimbali na wasikilizaji walikuwa nataka kujua nini
zaidi kilitokea kupitia kipindi cha Hekaheka, chanzo cha ugomvi hasa ni
nn?
Baada ya message nyingi sana kwenye kipindi cha hekaheka ilibidi
wahusika wanyanyue simu zao kuwatafuta Adam, Fetty na B12 kujua nini
kilichosababisha kuchapana makonde wakati bado kipindi kikiwa hewani.
Muhusika alinyanyua moja kwamoja simu na kumpigia B12 ambaye alikataa
kabisa kueleza chanzo cha sakata hilo la kutwangana huku akisema mambo
yote yapo kwa uongozi...
Simu ya pili ilimuendea ADAM MCHOMVU ambaye pia aligoma kuelezea
kilichotokea jana, baada ya Muda mfupi Adam alimkabidhi Dem wake ili
azungumze na mwandishi, huku akijua kwamba harikodiwi kumbe yupo hewani,
alikiambia kipindi cha hekaheka kwamba ADAM amemaind na hataki kuongea
na simu!!
Simu ya tatu ilienda kwa DJ FETTY, Ambapo iliita bila majibu kwamba ilikuwa haipatikani..
Chanzo kinasema kwamba baada ya ugomvi, vifaa mbalimbali vya studio
vimeharibiwa wakati wa ugomvi huo kama MIC, COMPUTER Meza nk. Endelea
Kufuatilia Hapa ili ujua ni hatua Gani watachukuliwa watangazaji hawa
kwa kukosa utovu wa Nidhamu....
Chanzo-tanzanianewz.com