

Marehemu Henry Lyimo enzi za Uhai wake
Kwa
mujibu wa habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba Mwandishi wa habari
na Mtangazaji maarifu wa kipindi cha Michezo cha redio Moshi FM ya
mkoani Kilimanjaro Henry Lymo maarufu pia kwa jina la Kipese amefariki
dunia usiku huu.
Meneja
wa Vipindi Redio Moshi FM Yusuph Mazimu amesema mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika hospitali ya Kilema, Marangu Moshi.
Marehemu Henry Lymo mwenye tisheti nyekundu enzi za uhai wake akihojiwa na Mtangazaji wa sasa wa Kahama fm Halid Mchopa
Inasemekana
Kipese amepata ajali ya pikipiki kwa kugogwa na gari wakati akitoka
kuchezesha mechi ya mpira wa miguu maeneo ya himo mkoani Kilimanjaro.