WEZI WAIBA BEGI LENYE CHATU WAKIDHANI NI PESA JIJINI DAR, WATIMUA MBIO NA KUMTELEKEZA

Dar: Wezi waiba begi lenye chatu wakidhani pesa Mwenye nia mbaya anaweza kudhani amepata kumbe amepatikana, anaweza ukadhani kila siku atapiga bingo kama hatakamatwa na raia kumbe mzigo alioiba unaweza kugeuka fimbo na hatari kubwa kwake hata bila kukamatwa.

Watu wasiojulikana wanasadikika kuiba begi kubwa maeneo ya Sinza, Dar es Salaam wakidhani begi hilo lina pesa na badala yake wakakutana na chatu mkubwa walipolifungua.

Wakazi wa Sinza walimkuta chatu huyo katika daraja akiwa karibu na sanduku hilo linaloaminika kuwa lilimbeba chatu huyo. 

Inaelezwa kuwa wezi hao walilitupa begi hilo na kutokomea pasipojulikana baada ya kuona mambo yamekuwa ndivyo sivyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo