Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa katika jaribio la
kutaka kupora fedha kwa mmoja wa wateja aliyekuwa ndani ya benki ya NMB
tawi la uwanja wa ndege,wakiwa na pikipiki aina ya Boxer wameuawa na
wananchi waliamua kujichukulia sheria mkononi,huku jeshi la polisi kanda maalumu ya
Dar-es-Salaam likiwashikilia watu watatu mmoja akiwa ni mganga
aliyekuwa akiwatibu kwa nguvu za giza na kudai kuwapa nguvu.
Kamanda wa polisi kanda ya maalumu ya
Dar-es-salaam,kamishana wa polisi Selemani Kova amesema kuwa,watuhumiwa hao wa ujambazi walipoteza maisha mara baada ya kipigo na kupoteza maisha wakiwa
njiani kupelekwa hosipitalini,ambapo amesema katika tukio hilo walikutwa na bastola waliyotumia kurushiana risasi na polisi.
Jeshi la polisi limezitaka taasisi za kifedha kama
mabenki na taasisi na watu binafsi kuacha mtindo wa kubebeba fedha kwa
njia ya mifuko ya plastiki maarufu kama rambo,kubebea kwenye pikipiki na
aina nyingine za usafirishaji fedha ambazo zinatoa vishawaisi kwa watu
wasio na nia njema kuleta hujuma.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia wamesema
kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakikimbia hovyo huku wakirusha risasi
hewani, ambapo wamelishukuru jeshi la polisi kwa kudumisha doria na
kulitaka jeshi hilo kushirikiana na wananchi ili kuhakikisha kuwa
vitendo vya uporaji hasa kwenye mabenki vinakomeshwa.

