WATU 10 wamekufa katika matukio tofauti mkoani Mbeya likiwemo la mtoto
mdogo, Joshua Shukrani (3), kugongwa na gari na mwanafunzi wa shuleya
msingi Iduda, leus John (07), kufa kwa kugonhwa na gari alipokuwa
akivuka barabara.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ahmed Msangi, kwa vyombo vya habari Juni 9-13, 2014 ( tunayo nakala) imesema matukio hayo yametokea katika kipindi hicho na kuwataja waliokufa kuwa ni pamoja na, William
kabinji (38) mkazi wa kijiji cha mantengu ‘A’ alikutwa ameuawa kwa
kukatwa na kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa kuwa ni panga sehemu za
usoni na kisha kunyongwa na kutundikwa juu ya mti, Juni 08, 2014 katika kijiji cha Ilembo Wilaya ya Mbozi.
Amesmea inadaiwa kuwa chanzo cha
mauaji hayo ni kulipiza kisasi baada ya marehemu kuchoma moto nyumba
tatu za jirani zake na kuiteketeza nyumba ya, Elias mwamlima (32), Juni
04, 2014 na kutoroka na Ezekiel Kyando (72) mkazi wa Bagamoyo katika
Wilaya ya Tukuyu aliyekufa kwa kugongwa na gari na dereva asiyefahamika
mkazi Juni 8, 2014 saa 10:00 asubuhi.
Kamanga Msangi aliendelea kwa kuwataja wengine
kuwa ni, Petro Kibona (30), aliyekufa kwa kushambuliwa kwa kupigwa
sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamua
kujichukulia sheria mkononi wakitumia silaha za jadi mawe, fimbo na
rungu tukio lililotokea Juni 10, 2014 saa 3:00 asubuhi kwa tuhuma za
wizi wa pikipiki namba T.994 ARB aina ya Toyo, mali ya, Aron Baned (36)
ambayo hadi sasa inashikiliwa kwa uchunguzi.
"Juni 10, 2014, Wolter Jonathan (36)
mkazi wa morogoro amekufa papo hapo baada ya kugongwa na gari na dereva
asiyefahamika katika barabara Kuu ya Mbeya/Njombe katika kijiji cha
Mbuyuni, Wilaya ya Mbarali mkoa wa mbeya ambapo chanzo cha ajali
kinachunguzwa, alikimbia na gari mara baada ya tukio, na mwanafunzi wa
darasa la kwanza katika shule ya msingi Iduda Leus John (7) alikufa papo
hapo Juni 10, 2014 baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Coaster
lililokuwa likiendeshwa na dereva asiyefahamika
na kukimbia baada ya
tukio” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Hata hivyo, Mwanaume asiyefahamika jina wala makazi (30-35) aliuawa kwa
kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi
waliojichukulia sheria mikononi wakitumia silaha za jadi fimbo, mawe na
rungu kutokana na tukio la unyang’anyi wa pikipiki tukio lililotokea
Juni 11, 2014 saa 11: oo jioni katika kijiji cha Idiga Wilaya ya
Kipolisi Mbalizi.
Uchunguzi wa kipolisi umeonyesha kuwa
marehemu alimkodi mwendesha pikipiki yenye namba T773 CDJ aina ya
T-better, Imani Emanuel (19), na walipofika mbele zaidi ndipo
alijitokeza mtu mwingine na kwa pamoja walinyang’anya pikipiki na kisha
kumfungwa mikono na miguu kwa mipira na kutoweka na pikipiki hiyo ambapo
katika tukio jingine, Madawa Jaston (29), aliuawa kwa kuchomwa kisu
kichwani, usoni na miguuni na mumewe, Joseph John (49) wote wakazi wa
kijiji cha Isangati.
Katika tukio lingine, Rashid
Mfinanga (37) ‘dereva’ na Godeni Katemu (60), wamekufa baada ya gari
lenye namba T.254 BFZ aina ya Mitsubishi fuso lililokuwa likiendeshwa na
dereva Rashid Mfinanga, kupinduka na kuwaua papo hapo katika Wilaya ya
Kipolisi Mbalizi, na Mtoto mwenye umri wa miaka (3) Joshua Shukrani
mkazi wa Ilemi kufa kwa kugongwa na gari lisilofahamika namba za usajili
mara moja.
Taarifa za msako
Watu wawili, Braun kamwela (30), na
Gabriel Mwambene (30), wote wakazi wa Kiwira wakiwa na TV aina ya
Panasonic moja na Redio aina ya Sony mbili mali inayodhaniwa kuwa ya
wizi.
watuhumiwa walikamatwa juni 09, 2014 saa 9:00 usiku katika eneo la
kiwira, Kata ya Kiwira, wilayani Rungwe na taratibu za kuwafikisha
Mahakamani zinafanywa na Samson Julius (18), akiwa na bangi kete 68 sawa
na uzito wa gramu 340 mkazi wa kijiji cha NondeJuni 8.06.2014 saa 11:00
asubuhi katika eneo la stendi kuu ya mabasi, kata na tarafa ya Sisimba.
“Juni 10, 2014 tulimshikilia Asajile
Mwakisambwe (41) mkazi wa kijiji cha majengo kwa kosa la kukutwa na
pombe haramu ya gongo yenye ujazo wa lita 52, na mfanyabiashara Jailos
Jayange (45) mkazi wa Mbozi ameshikiliwa na Jeshi hilo Juni 12, 2014
akiwa na vipodozi mbalimbali vilivyopigwa marufuku na serikali katika
Wilaya ya Momba.
Wakutwa na note bandia
Watu watatu, Tatu Mwampashi (25),
Angomwile Kapungu (26), wakazi wa mtaa wa Mnyamwanga wanashikiliwa
wakiwa na noti bandia 62 kila moja ikiwa na thamani ya Tshs 5,000 sawa
na Tshs 310,000 zote zikiwa na namba AA0845926 Juni 12, 2014, na
mtuhumiwa mwingine Angomwile Kapungu (26) alikamatwa katika Kitongoji
cha Sikanyika, Kata na Tarafa ya Tunduma, Wilaya ya Momba, akiwa na dola
bandia 2 kila moja ikiwa na thamani ya USD 100 zikiwa na namba
BL-72830434-a na FT-85311229-h na taratibu za kuwafikisha Mahakamani
FiktaPevu imejulishwa kuwa zinaendelea.
Wapiga debe tisa mbaroni
Jeshi hilo, linawashikilia watu tisa
kwa tuhuma za kufanya fujo maeneo ya Stendi ya Mabasi Ilomba jiji humo
kufuati mgomo wa daladala Juni 10, 2014.
Watuhumiwa hao ni pamoja na, Ipyana
Mwangomole (27), Hussein Hassan (32), Zakaria lianda (23), Bahati
Mathias (28), Boniface Jasson (22), Amos Robert (16), Otto Jeki (21),
Alex mwaikuji (28), na Leofasi Anthony (17), wote wakazi wa jijini humo
ambao wanatuhumiwa kwa kosa la kufanya fujo kufuatia mgomo wa daladala
na taratibu za kufikishwa Mahakamani zinaendelea.
