Kamanda wa Polisi mkoani humo, Joseph Konyo, amehabarisha kuwa Juni
13, 2014 kuwa tukio hilo limetokea Juni 11, mwezi huu saa 4:45 asubuhi
ambapo mwanafunzi huyo akiwa na wenzake watatu wakitoka shule kufanya
usafi ,walipofika eneo hilo mwanafunzi mwenzao alienda kujisaidia karibu
na kisima hicho kinachomilikiwa na Marco Maico.
Amesema mara baada ya mwanafunzi huyo
alipomaliza kujisaidia ‘Marco’ alipita na kukuta kinyesi hicho na
kuanza kumuamuru kuwa azoe kinyesi chake kwa mkono na kukitupa na baada
ya kukitupa alimuamuru mwanafunzi huyo kukichukua na kukila hadi
kiishe. Aidha, kutokana na hofu ya mwanafunzi huyo kuogopa kupigwa, alilazimika
kukila huku wenzake wakimsubiri na baada ya kumaliza alienda nyumbani na
wenzake.
Baada ya kufika nyumbani mwanafunzi
huyo alimwambia Mama yake, Agnes Lujaja (26), juu ya tukio hilo ndipo
Mama yake alipoenda kuripoti tukio hilo kwa balozi wa nyumba kumi kutoa
taarifa na kupewa barua ya kumpeleka katika Zahanati ya Nyakabale kwa
matibabu.
“Mara baada ya huyo Mama yake na
mtoto kuripoti kwa Balozi wa nyumba kumi, ilikuwa bahati nzuri kwa kwa
maana waliwahi kuripoti katika Kituo cha Polisi kilichokuwa karibu nao
na ndipo tulipofuatilia tukio hilo kwa ukaribu na kufanikiwa kumkamata”
alisema Konyo.
Hata hivyo, amesema baada ya Jeshi la
Polisi kufuatilia tukio hilo waliweza kumkamata mtuhumiwa ambaye hadi
sasa anashikiliwa kwa upelelezi zaidi na kusema mara baada ya upelelezi
kukamilika sheria itachukua nafasi yake.
chanzo:fikrapevu
