Tuzo za watu za Tanzania au Tanzania People's Choice Awards zitatolewa
leo kwenye ukumbi uliopo Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
Jumla ya
vipengele 11 vinashindaniwa na nominee watatu katika kila kimoja
wameingia fainali.
Mshindi katika kila kipengele atapewa zawadi ya
shilingi milioni moja pamoja na trophy.
Host wa tuzo hizi ni mtangazaji
mkongwe wa radio, Jimmy Kabwe.
Pamoja na burudani mbalimbali
zitakazokuwepo, video mpya ya Ben Pol ya wimbo wake ''Unanichora'' aliomshirikisha Joh Makini itazinduliwa.