Muimbaji kutoka Mombasa, Kenya Nyota ndogo amejikuta katika hali ya
wasiwasi baada ya kukutwa na mkasa wa karne hivi karibuni.
Nyota ameelezea kilichomkuta baada ya kuingia kwenye chumba cha hoteli
ili abadili nguo, na kwa bahati mbaya alivua nguo zake mbele ya kioo cha
chumba hicho bila kujua kioo hicho upande wa nje kinaonesha live bila
chenga.
Kupitia akaunti yake ya Facebook Nyota Ndogo ameelezea kilichomsibu: 'yani nimekwenda show.nikapewa chumba chakubadili nguo.nimevua nguo
zote najipaka mafuta pole pole kumbe najiangalia kwa kioo kumbe upande
wapili naoneka kila kitu.yani nimekosa amani"aibu nilio iona mungu ndio
anajua.sijui wamechukua video..haya ngoja tusubiri".
Hata hivyo Nyota amewapunguza wasiwasi mashabiki wake walio comment
kumpa pole kwa kusema alibakiwa na nguo za ndani wakati hayo yanatokea. "hapana nilibakisha cha ndani na nyonyo ilikua na nguo pia.kitu sielewi
ni alienipeleka kubadili nguo ina maana hakujua nje naonekana?maana
aliambia kioo hiki jiangalie mpaka miguu."
Nyota ameamua kuwapa taarifa mashabiki wake mapema ili endapo kama kuna
aliyerekodi na video ya tukio hilo ikisambaa watu wafahamu kilichotokea.
>>>BONGO 5