MWIMBAJI WA KIKE WA NIGERIA ATANGAZA KUWAPA NGONO BOKO HARAM ILI WAWAACHIE HURU WASICHANA 200 WALIOWATEKA



Mwimbaji wa kike wa Nigeria mwenye umri wa miaka 23 anaefahamika kwa jina la Adokiye ameeleza anachofikiria kuhusu wasichana zaidi ya 200 wanaoshikiliwa na kundi la Boko Haram.
 
Mwimbaji huyo ambaye anafahamika sana kwa comments  zinazotengeneza mijadala hudai kuwa yeye ni bikira.
Mwishoni mwa wiki hii ameiambia Showtime kuwa anajitoa yeye kwa kundi la Boko Haram kama inawezekana wao kuwaachia wasichana wanaoshikiliwa na kundi hilo.
 
“Sasa hivi ni saa tato usiku, je unajua ninachofikiria? Wale wasichana wadogo, wapi walipo na nini kinawatokea muda huu. Sio sawa. Ni wadogo sana. 

"Nawishi ningeweza kujitoa mimi kubadilishana nao. Wana umri kati ya miaka 12 hadi 15. Mimi ni mkubwa na nimeshazoea maisha zaidi yao. 

"Hata kama wanaume 10 hadi kumi na mbili watanichukua kwa usiku mmoja, sijali. Nachojali wawaachie hao wasichana warudi kwa wazazi wao.”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo