MWANAMUZIKI HAFSA KAZINJA ABADILI DINI, KISA ANASUMBULIWA NA MARUHANI

Mwanamuziki Hafsa Kazinja anayetamba na Wimbo wa Mlala Nje huku video yake ikiwa tayari, ameamua kuikacha dini yake ya Kiislam na kuhamia kwenye Ukristo.Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Hafsa alisema alifikia uamuzi huo baada ya kusumbuliwa na maruhani ambayo yalimfanya arukwe na akili.

“Niliumwa sana hadi ikaonekana nimerukwa na akili, maruhani ndiyo yaliyokuwa yananisumbua. Kuna kipindi yalikuwa yakiniambia nisile samaki wala dagaa, mara yakaniambia natakiwa kuwa mganga.

“Njia zote ziligonga mwamba, nikaambiwa nisali na nimuachie Mungu, nikawa nikisali sauti zinanijia nimtukane  Mungu tena matusi makubwa, nimeenda hadi kwa waganga, mashehe na walokole wakaniombea na nikapoteza pesa nyingi hadi nikauza nyumba yangu na magari lakini wapi. Nimekwenda Kanisa la Zoe ndiyo nimepona, namshukuru Mungu.

“Sasa nimeamua kuwa Mkristo, yaani nimebadili dini kwa kumaanisha, nampenda Mungu katika roho na kweli.

Sijabatizwa hivyo bado sijabadili jina ila nasali Kanisa la Zoe lililopo Segerea jijini Dar.”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo