Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo la kinyama, Kaimu
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Koka Moita, alisema tukio la ubakaji lilitokea
wilaya ya Karatu, mkoani Arusha, kabla ya kufariki kwake mjini Moshi.
Alisema wakiwa huko Mang’ola baba huyo aitwae Elisha Wazaeli,
(38), alimbaka mtoto huyo kabla ya kurudi nae nyumbani kwao Arusha na kwamba
alipofika Arusha alikorofishana na mke wake ambae ni mama wa mtoto huyo.
Aliendelea kusema kuwa pamoja na kupewa dawa lakini homa hiyo
iliendelea kumuandama mtoto huyo na baada ya mamake kumhoji zaidi alimwambia
mamake ya kuwa babake alimbaka.
Kaimu Kamanda Moita aliendelea kusema kuwa polisi walimchukua
mtoto huyo na kumpeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi pamoja na tiba
katika hospitali ya Mkoa ya Mawenzi hadi alipofariki dunia Juni 4, mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda huyo, mtuhumiwa wa tukio hilo
ametoroka na kwamba tayari jeshi la polisi mkoani humo limeanza msako wa
kumtafuta ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake.
Aidha Kaimu Kamanda Moita alitoa wito kwa akina mama
kuhakikisha wanakuwa karibu na watoto wao badala ya kuwaachia wafanyakazi wa
nyumbani jukumu hilo muhimu katika malezi ya watoto.