MWIGIZAJI mwenye figa ya aina yake Bongo Movie, Tamrina
Posh ‘Amanda’ ameamka na kushtuka akiwa amechanjwa chale na watu
wasiojulikana kama alivyowahi kufanyiwa marehemu Recho.
Akizungumzia tukio hilo, Amanda alisema lilitokea siku ambayo dairekta
mkongwe nchini George Tyson alipofariki dunia (Mei 30) ambapo hakujua ni
nani aliyemfanyia ‘unyambilisi’ huo usiku kwani alishtuka asubuhi na
kuona akivuja damu zikiashiria kuchanjwa kwa wembe.
“Nilijikuta nimechanjwa lakini Mungu ni mwema, waliofanya hivyo kama
walikuwa na nia mbaya, wameshindwa kwani nilikwenda kuombewa kanisani
halitanipata lolote,” alisema Amanda.