MKUU WA WILAYA AKANUSHA TAARIFA ZILIZOTANGAZWA KUWA MKUU WA MKOA WA GEITA AMEPATA AJALI YA GARI

UONGOZI wa serikali mkoani hapa, umesema hakuna ajali iliyotokea ikihusisha msafara wa Mkuu wa Mkoa, Said Magalula na kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa, Severine Kaitwa.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya (DC) ya Geita, Omar Mangochie, alisema taarifa zilizochapishwa katika gazeti la Tanzania Daima Jumatano, toleo la Juni 15 hazikuwa sahihi.

Mangochie alisema licha ya kutokuwepo kwa ajali, hata mkuu wa mkoa yupo China tangu Juni 9, mwaka huu.

“Hii habari imetushangaza na kutuletea matatizo maana viongozi wetu wote wapo salama na hakuna msafara wala ajali iliyotokea kama mlivyoandika.

“Inaonekana aliyetunga uongo huu na kuutuma kwenu ana nia ovu kwa viongozi wa serikali,” alisema Mangochie.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo