Mwajuma
Bakari Tindwa mwenye umri wa miaka 52, mkazi wa Mwembesongo aliyemleta
mganga akiandaliwa dawa ili kumrejesha mtoto aliyepotea.
MGANGA mmoja wa jadi, hivi karibuni alikusanya umati
mkubwa wa watu baada ya kuinyeshwa dawa familia nzima ya mwanamke
aliyemleta kwa lengo la kumfanyia uganga ili kumrejesha mtoto wake
aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha mjini hapa.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi ya wiki iliyopita baada ya Mwajuma
Bakari Tindwa mwenye umri wa miaka 52, mkazi wa Mwembesongo kumleta
mganga huyo, Omar Ally ili amrudishe mtoto Omar Abdul Matenda (10),
mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Uhuru, aliyepotea
Juni 8, mwaka huu.
...Bi. Mwajuma Bakari Tindwa akinywa dawa hiyo.
Mwajuma aliliambia gazeti hili kuwa mwanaye alipotea katika mazingira
ya kutatanisha na kwa zaidi ya wiki tatu, wamekuwa wakimtafuta bila
mafanikio.
...mmoja wa ndugu wa familia akipata dawa.
“Baada ya kumkosa kote huko nilitoa ripoti Kituo cha Polisi Msamvu na
kituo kikuu cha polisi nao wamehangaika bila mafanikio, baada ya
kujadiliana na familia yangu tuliamua kumchukua huyu mganga ambaye
alituhakikishia kumrejesha mwanangu,” alisema.
...Hata mtoto mdogo naye alishiriki kikombe cha dawa kutoka kwa Sangoma.
Alipotakiwa kuzungumzia mazingira ya mtoto
huyo kupotea, alisema alikuwa akicheza na mwenzake ambaye pia anaitwa
Omar, lakini mwenzake alirudi na kudai rafikiye amepotea kiajabu.
Mganga huyo aliyefika hapo akiwa na timu ya watu wanne, alisababisha
umati wa watu kujaa kushuhudia alichokuwa akikifanya, ikiwa ni pamoja na
kumchinja paka na kuinywa damu yake, kuchimba shimo mithili ya kaburi
nje ya nyumba na kufukia msalaba.
...Timu nzima ya waganga waliofika kutoa huduma kwa Bi. Mwajuma Bakari Tindwa ili kumrejesha mtoto aliyepotea.
Aidha, akitumia kifaa kama darubini, alimulika na kwenda nyuma ya
nyumba ambako alichimba na kutoa mapembe mawili, vitu ambavyo hata
hivyo, havikuwezesha kurejea kwa mtoto huyo.
Sangoma hao wakiwa na picha za maraisi wa awamu zote tatu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Tulipofika hapa mtoto alikuwa jirani kwa mujibu wa vifaa vyangu,
lakini sasa wamempeleka umbali wa mita 250 hivyo kwa sasa tunaingia
ndani na kufanya shughuli zetu kwenye nyumba hii na baadaye tutaendelea
na kazi ya kumrejesha,” alisema mganga huyo baada ya kuona sura za watu
zikiwa kama zinazouliza.
Mganga akifanya vitu vyake kwenye shimo alilochimba nyuma ya nyumba.
Katika hali ya kushangaza, mganga huyo alikutwa akiwa na picha za
marais watatu wastaafu, Baba wa Taifa na Ali Hassan Mwinyi sambamba na
ya Rais Jakaya Kikwete. Hadi Uwazi linaondoka eneo la tukio, mtoto Omar
hakuwa amepatikana.
CHANZO:GAZETI LA AMANI
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi