MAJANGA NIGERIA: MLIPUKO MWINGINE WAUA 18, WENGINE 19 WAKIJERUHIWA

WATU 18 wamepoteza maisha huku zaidi ya 19 wakijeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea mji wa Mubi nchini Nigeria jana jioni. 

Polisi nchini humo wamethibitisha kutokea kwa mlipuko huo.
 
Inadaiwa kuwa mlipuko huo ulilenga chumba kimoja cha burudani ambapo watu walikuwa wakitazama mechi ya soka kwenye televisheni.

Mpaka sasa hakuna kundi lolote lililothibitisha kuhusika na shambulio hilo japo polisi wanadai yawezekana ni kundi la Boko Haram.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo