Mahakama moja nchi Misri imemtia hatiani dereva mmoja wa Taxi na
kumpiga faini ya paundi 5,000 za nchi hiyo ni sawa na Sh. Milioni moja
ya Tanzania, baada ya kumwita mwanamke demu.
Dereva huyo
alikumbwa na mkasa huo wakati akiwa katika mishemishe zake za kawaida
ndipo alipokutana na maandamano ya wanawake wanaopinga kitendo cha
kubakwa mwanamke mweziwao na kundi la vijana wiki mbili zilizopita
katika uwanja wa mapinduzi jijini Cairo.
Dereva huyo akiwa ndani ya gari yake alikutana na wanawake hao na
kumwambia mwanamke mmoja aliyekuwa mbele yake wasaa ya muza (pisha wewe
demu) kauli ambayo imetafsiriwa kuwa ni ya unyanyasaji wa kijinsia.
