Wakazi wa Tabata Kinyerezi wamekosa mawasiliano na maeneo mengine ya
jiji baada ya lori lililobeba tani arobaini kutumbukia kwenye daraja la
Segerea lenye uwezo wa kupitisha tani saba .
Lori hilo likiwa limebeba matofali na kudaiwa kuwa
na abiria sita ambao wawili wanasemekana kupoteza maisha na wanne wakiwa
wamejeruhiwa vibaya baada ya dereva kukatazwa kupitisha lori hilo
lenye tani 40 ambapo kibao kinaonyesha tani 7.
Wananchi wa Kinyerezi wameiomba serikali
kumchukulia hatua kali dereva huyo ambae amesababisha hasara kubwa ya
miundombinu ya serikali licha ya kukatazwa na wakandarasi .
Mkandarasi wa daraja hilo amekiri kutokea kwa ajali
hiyo na wanachokifanya sasa ni kuweka daraja la muda ili wananchi
waweze kupita.
