KOCHA MBRAZIL MARCIO MAXIMO ASAINI MKATABA NA YANGA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghGLUksp6VP9xzLz2O_izP_LUe2B191I9uKZIss5rRGja2ss0HxZa7zMLPmbnfEhJVJotvnLl51HoXSfmTEH2vSYxDrkCczQs8RAEWh1cxeo2vZnKzC9xApBygUEheWXJeqepRHtdiuwI/s1600/maximo3.jpg 
Kocha mkuu wa zamani wa timu ya Taifa, taifa Stars Marcio Maximo amesaini mkataba  wa kuwa kocha mkuu na timu ya Yanga kwa muda wa miaka miwili. makubaliano hayo yamefikiwa jana, wakala  anaye mwakilisha Ally Mleh wa kampuni ya Manyara Sports Management amethibitisha hilo.
"Ni kweli kocha Marcio Maximo amekubali kuingia mkataba na timu ya  Yanga ambapo anatarajiwa kuanza kazi rasmi tarehe 27/06/2014 ambapo  atafuatana na msaidizi wake Leonardo Neiva. Mazungumzo ya makubaliano   hayo yalichukua muda mrefu kidogo hatimaye tumefikia
makubaliano.Tunashukuru mungu kila kitu kimekamilika.

Kwa niaba ya Marcio Maximo napenda kuushukuru uongozi wa klabu ya Yanga, shukrani za pekee kwa mwenyekiti wa Yanga ndg Yusuf Manji na makamu wake Clement Sanga,  kwa kweli wameonyesha  umakini na professional kwa muda wote wa  majadiliano. Nawaomba wachezaji,wanachama na wapenzi wote wa yanga tumpe ushirikiano.

Baada ya kumaliza mkataba wake wa kuifundisha Taifa Stars nchini aliingia mkataba na timu kubwa nchini brazil  mpaka mkataba wake ulipoisha.Kwa wakati huu kulikuwa na mazungumzo na timu mbalimbali Zilizotoa  ofa nchini China, Ethiopia na Afrika kusini lakini Yanga wamefanikiwa kumnasa kocha huyo.

Maximo anatarajia kuwasili LEO siku ya Alhamis saa saba mchana

Maximo ilikuwa awasili nchini baada ya fainali za kombe la dunia lakini kutokana na mkataba alioingia na Yanga imebidi afupishe mkataba wa kazi ya 'commentator' aliyokuwa akiifanya nchini Brazil ili awahi kuandaa program zake Yanga.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo