Wananchi
wa Kijiji cha Kitwai A wakiwa wamenyoosha mikono juu,kwenye mkutano wa
hadhara,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akimuunga mkono
jambo Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh Christopher Ole Sendeka,katika
suala zima la Utekelezaji wa Ilani ya CCM .
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua gari la mradi wa
Kukodisha la Kikunndi cha Vicoba Mkombozi chenye wanachama wapatao
30,mjini Orkesument,Wilayani Simanjiro mkoani Manayara.
Kinana
ameambatana
na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,wako moani Manyara kwa
ziara ya siku saba ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo
inayotekelezwa kwa
kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za
mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.
Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh Christopher Ole Sendeka,akiwahutubia baadhi ya Wananchi
wa Kijiji cha Kitwai A,akiwa ameambatana na msafar wa Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana,Katika kijiji hicho Ndugu Kinana alizindua Ofisi ya
Mtendaji Kata ya CCM Kitwai A,na kuahidi kujenga shule ya Sekondari kwa
ajili wananchi hao ambao hapo awali walikuwa na shule za msingi tu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana akipata maelezo mafupi kutoka
kwa Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh.Ole Sendeka wakati akiangalia josho
la ng'ombe la Orkirung'rung ambapo kuna mradi wa ufugaji wa ng'ombe chotara
ambao ni ufugaji wenye tija na unasaidia sana kuongeza thamani mifugo.