Halmashauri
ya mji mdogo wa Mombo imetunga sheria ndogo ya kuwabana wenye mabasi
kudhibiti abiria wao wasitupe taka hovyo hasa za mabaki ya vyakula
wanapaokuwa katika maeneo ya miji ili kuepuka uchafuzi wa mazingira
unaofanywa na baadhi ya wasafirishaji na kuhatarisha afya za wakazi wa
maeneo yaliyopo pembeni mwa mji huo.
Akihutubia wakazi wa mji mdogo wa Mombo katika zoezi la usafi wa
kujitolea uliofanywa na kikundi cha Fahari Sanaa Group cha mji mdogo wa
Mombo,mwenyekiti wa mamlaka ya mji huo Bwana Richard Luizile (PICHANI)amesema
ameshatoa taarifa kwa afisa afya kuwaita mawakala wa kampuni za magari
ya abiria kwa ajili kuwapatia wenye mabasi nakala ya sheria hiyo ambayo
inaagiza kuwa kila mwenye basi lazima awe na chombo maalum cha
kuhifadhia taka.
Amesema endapo baadhi ya abiria ambao watabainika kutupa taka hovyo
kupitia dirishani hasa anapokuwa katika maeneo ya miji wahusika wa
chombo cha usafiri watatozwa faini ya shilingi 50,000/= kila basi
litakalobainika kukiuka sheria hiyo kwa abiria wake kutupa taka hovyo
watahakikisha wanawadhibiti watuhumiwa kupitia askari wa jeshi la polisi
waliopo katika njia kuu ya kwenda mikoa ya kilimanjaro na Arusha ili
kuhakikisha kuwa suala la uchafuzi wa mazingira linadhibitiwa.
Kwa upande wake mratibu wa usafi wa maji mdogo wa mombo ambaye ni
mwenyekiti wa taasisi ya Fahari Sanaa Group Bwana Hamis Ngota amesema
suala la usafi halibagui itikadi,vikundi wala mkubwa kwa mdogo na badala
yake ni kazi ya kila mmoja anapaswa kuzingatia sheria na taratibu za
usafi katika eneo lake.
