HALI BADO NI MBAYA KENYA, AL SHABAAB WATUHUMIWA KUUA WATU WENGINE 10 HUKO LAMU



Shambulizi  jingine limetokea katika eneo la Mpeketoni karibu na Lamu , pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya watu 10.
 
Shambulizi la leo limetokea siku moja tu baada ya Al Shabaab kukiri kufanya mashambulizi yaliyowaua watu 50 Jumatatu.
Polisi wanasema kuwa washambuiaji hao walivamia kijiji kimoja usiku kucha. 
 
Kundi la Al Shabaab lilikiri kufanya mashambulizi hayo na kuambia shirika la Reuters kuwa operesheni yao ya mashambulizi itaendelea nchini Kenya.
 
Takriban watu 50 waliuawa katika mashambulizi yaliyofanyika usiku wa kuamkia Jumatatu huku washambuliaji wakishambulia hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari.

Credit: BBC


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo