SAKATA la tuhuma za ubakaji zinazomkabili mume wa Flora Mbasha sasa limechukua sura mpya baada ya maovu yao mengine kuanikwa hadharani na ndugu wa Flora.....
Msichana
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Cathy ambaye ni dada binamu
wa Flora amedai kuwa kinachowatafuna wawili hao ni laana
waliyoipata kutoka kwa babu wa Flora, marehemu baba Askofu
Moses Kulola.....
Ndugu
huyo wa Flora amesema kuwa wawili hao waliwahi kufikia
nyumbani kwa askofu Kulola huko Mwanza,siku chache kabla ya
Kulola kuaga dunia na kufanya madudu mengi ikiwemo kuingiza
askari polisi kwenye chumba cha Kulola....
Ndugu
huyo alidai kuwa wawili hao walifikia hatua ya kuingiza
askari kwenye chumba cha askofu Kulola kwa madai ya kuibiwa
sh. 300,000 ( Laki tatu ) za Emmanuel Mbasha, mume wa Flora
huku wakimwaga matusi mazito kwa wajukuu wa Kulola....
"Walifikia
pale kwa babu, yule Mbasha akawa na pesa kama laki tatu hivi,
akazihifadhi kwenye nyumba ndogo ya chini waliyofikia,nyuma ya
nyumba ya babu, akawa amesahau alikoziweka zile pesa basi
wakaanza kuwatukana matusi ya nguoni wajukuu wa babu pale kama
hawana akili nzuri, yeye Mbasha na Flora," alisema ndugu huyon wa Flora.
Akaendelea
kudai kuwa walipoona hakuna ushirikiano kwa wajukuu wa babu
wakaamua kuita polisi waliofika pale nyumbani na kuanza kufanya
upekuzi wa nguvu kwenye kila kona ya nyumba ya baba
Askofu....
"Walipoona
hawajafanikiwa kuzipata akaamua kuwaingiza polisi mpaka chumbani
kwa babu, na babu alikuwa hayupo nyumbani, alikuwa kanisani,
sasa aliporudi ndipo alikuta askari chumbani kwake wakifanya
upekuzi. Babu alikasirika sana na kujikuta akimwaga machozi," alisema Cathy
Akaendelea
kudai kuwa babu alishangaa sana kufikia hatua ya wawili hao(
Flora na mumewe) kutomwamini hata yeye mpaka kuingiza askari
ndani ya chumba anacholala lakini wawili hao walimpuzaa hata
baba Askofu huyo....
"Babu
aliwalaani wale na aliwaambia kuwa siku si nyingi maovu na
uchafu wao utajulikana kwenye jamii huko Dar wanakowaibia watu
kwa kujifanya wameokoka wakati siyo kweli na wanatapeli watu
kila siku,akasema wataishia pabaya muda si mrefu," alisema Cathy.
Akaendelea
kudai kuwa Flora na mumewe hawakuwahi kuomba radhi kwa babu
yao Askofu Kulola mpaka alipofariki, na mpaka leo hii laana
yake bado inaawatafuna sana na haya yanayoendelea ni matokeo
ya laana hiyo.
