MKURUGENZI wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’
Asha Baraka, amesema kamwe hawezi kumsamehe mwanamuziki Ally Choki
ambaye ni Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, ambaye ana bifu naye la
muda mrefu.
Hivi karibuni habari zilienea kuwa wawili hao wameshapatana baada ya
kukutanishwa na chombo kimoja cha habari nchini, jambo ambalo Asha
amelikanusha.
“Siwezi kupatana na Choki kwa sababu sioni haja ya kufanya hivyo.
Nimesikia kwenye mitandao kuwa eti tumepatanishwa... watu bwana! Labda
waliopatana ni wao siyo mimi. Nasisitiza habari hizo ni za uongo na
ninaomba Choki akae mbali na mimi,” alisema Asha.
Kwa upande wa Choki, alipoelezwa kuhusiana na majibu ya Asha, alicheka
kisha akasema: “Kama yeye amesema hivyo, acha iwe hivyohivyo. Kwanza
hayo mapatano yenyewe sijafanya kwa ajili yake maana hakuna kitu
ninachotaka kwake. Nina mambo mengi ya kufanya.”