
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kushoto) akizuliwa na Mawaziri
na Manaibu Waziri kutomfuata Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila
baada ya kupandwa na hasira kufuatia mbunge huyo kumtuhumu kwa kumuita
mwizi kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin
Mjwahuzi
-----
-----
Kama
siyo kuzuiwa na mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji
Frederick Werema jana angezua tafrani bungeni kutokana na kitendo chake
cha kutaka kumpiga Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David
Kafulila.
Sakata
hilo lilitokea jana asubuhi baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan
Zungu kuahirisha kikao cha Bunge hadi jioni, ikiwa ni muda mfupi baada
ya Werema na Kafulila kurushiana maneno bungeni. Jaji Werema alichukia
baada ya Kafulila kumwita mwizi, akijibu mapigo baada ya mbunge huyo
kuitwa tumbili na mwanasheria huyo.
Waliomzuia
ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira, Waziri wa
Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene na Naibu Waziri wa Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Dk Abdulla Juma Saadallah. Mawaziri hao
walimsindikiza Werema hadi nje ya Ukumbi wa Bunge na kutoweka.
Ilivyokuwa
Hali ilianza kuchafuka wakati Jaji Werema alipokuwa akijibu mwongozo uliombwa na Kafulila kuhusu fedha za akaunti ya Escrow.