WIZARA YA ARDHI,NYUMBA NA MAKAZI YAZUA GUMZO BUNGENI

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeitaka serikali kusitisha zoezi la ugawaji wa ardhi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi mpaka pale itakapobainika ni kiasi gani cha ardhi kilichopo kwa wawekezaji,ili kuepusha migogoro ya ardhi nchini ambayo inaendelea kusababisha vifo vya watanzania wasio na hatia

Hatua hii inakuja huku waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka akikanusha vikalia uwepo wa migogoro ya ardhi kwa kile anachokiita ukosefu wa tekinolojia.

Ni katika Mkutano wa kumi na tano kikao cha ishirini Halima Mdee Msemaji kutoka Kambi Rasimi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni waziri kivuli wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi anasimama na kusema tathmiini hiyo ikifanyika kwa kiasi kikubwa itapunguza migogoro miongoni mwa wananchi na wawakezaji hasa wa kigeni

Esther Bulaya ni Mjumbe kutoka kamati yaBunge Maliasili na mazingira kwa niaba ya kamati hiyo anasistiza kufuata kwa sheria katika kutoa vibali vya ujenzi wa magorofa nchini.

Na hawa ni wabunge ,wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wamepata nafasi ya kuchangia.

Tarehe 27 mwezi huu waziri mwenye Dhamana ya wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Prof Anna Kajumulo Tibaijuka aliwasilisha makadirio ya Mapato na matumizi kwa wizara yake na akaomba shilingi bilioni 11.5 kwa ajili ya mishahara ,matumizi mengineyo bilioni 42.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo