Mwanamke
mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Christina Hayola(35), mkazi wa Kijiji
cha Lwalanje wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, amekutwa amekufa na mwili
wake kubainika kuwa ulikuwa na majeraha ya kukatwa katwa Kifuani,
kichwani na mguu wake wa kulia.
Unyama huo unadaiwa kufanywa na mumewe, Mussa Nsagaje, maarufu kwa jina la Mwaulambo.
Sababu
za mauaji hayo zinatokana na kile kinachodaiwa kuwa ni ugomvi wa
masuala ya wivu wa kimahusiano(Ngono) ulioanzia eneo la kilabu cha
pombe.
Mwili
wa marehemu ulikutwa katika Kijiji cha Magamba, kata ya Isansa, tarafa
ya Igamba, wilayani Mbozi, mkoani Mbeya na mtuhumiwa alitoroka baada ya
kutekeleza mauaji hayo.