Diwani
wa kata ya Mungaa Matheo Alex akizungumza kwenye hafla ya sala
kuwaombea watu waliopoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni
ya summary aprili 28 mwaka huu.Sala hiyo maalum,imefanyika jana eneo
ilikotokea ajali hiyo.
Mke
wa marehemu mwenyekiti wa kijiji cha Utaho Paulo Hamisi (41)
aliyefariki dunia kwa kugongwa na basi la Summry Aprili 28 mwaka huu.
Baadhi
ya wananchi wa kijiji cha Utaho tarafa ya Ihanja wilaya ya
Ikungi,waliohudhuria sala maalum ya kuwaombea ndugu zao 15 waliopoteza
maisha baada ya kugongwa na basi la kamuni ya summry Aprili 28 mwaka
huu.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Ikungi
WAUMINI wa madhehebu mbalimbali
ya dini wakazi wa kata ya Utaho tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi mkoa
wa Singid hivi karibuni wameungana na kufanya sala maalum katika
kuwaombea ndugu zao 15 waliofariki dunia baada ya kugongwa na basi la
kampuni ya summary.
Sala hiyo maalum imefanyikia
kando kando ya barabara kuu itokayo Singida – Dodoma eneo la kambi la
kampuni ya SIETCO kijiji cha Utaho ajali hiyo mbaya ilitokea Aprili 28
mwaka huu saa 2.45 usiku.
Akihubiri kwenye hafla hiyo ya
sala,Mchungaji wa kanisa la Free Pentekoste kijiji cha Utaho,Francis
Pius amewataka waumini wa dini mbalimbali na wananchi kwa ujumla
wazingatie sheria za usalama barabarani kama njia mojawapo ya kupunguza
ajali zinazochangia watu kupoteza maisha pamoja na mali zao.
Amesema baada ya kujengwa
barabara kwa kiwango cha lami ajali zimeongezeka mara dufu kutokana na
baadhi ya watu kutokuwa waangalifu na kwa kiasi kikubwa kutokutii sheria
za usalama barabara.
“Tabia ya watu kutokuzingatia
sheria za usalama babarani inachangia mwenye baiskeli kumdharau mwenye
pikipiki na mwenye pikipiki kumdharau mwenye gari kinachotokea ni kwamba
wananyang’anyana barabara na kusababisha ajali zinazopoteza maisha ya
watu na mali zao”alifafanua zaidi Mchungaji
Mchungaji huyo amesema makosa
ya aina hiyo,hayapaswi kufanywa na binadamu mwenye akili tofauti na
mnyama kwa hiyo tunapaswa kuzingatia matumizi sahihi ya barabara ili
kupunguza ajali.
“Tuwe makini wakati wa kuvuka
barabara na pia wakati tukivusha mifugo yetu tukifanya dharau barabarani
kuwa dereva wa gari,pikipiki na hata baiskeli eti atakuona ili
asikugonge tutakosea sana kwa sababu tutakuwa tunasababisha ajali kila
kukicha”,amesema Mchungaji Francis.
Akifafanua zaidi,amesema
barabara za kiwango cha lami ni nzuri na zina faida nyingi pamoja na
kuharakisha upatikanaji wa maendeleo,lakini tunapaswa tuzingatie
matumizi bora ya barabara ili tusiendelea kupukutika kwa ajali.
Naye Diwani wa kata ya Kituntu
(CCM),Naftali Gwae alikanusha uvumi kuwa Rais Jakaya Kikwete alituma
rambai rambi zikiambatana na fedha.
“Rais wetu alituma salama za
rambi rambi na wala sio fedha kwa hiyo ndugu zangu niwasihi tu kwamba
wakati huu mgumu unaoambatana na majonzi mengi yatasemwa lakini tuwe
makini na kuyafanyia uchunguzi kwanza”,amesema.
Aidha,uvumi ulioenea kwamba
Diwani wa CCM na Mtendaji wamechukua kutoka ofisi ya kijiji nyaraka za
benki zinazodaiwa kuonyesha kuwa kijiji hicho kina akaunti yenye zaidi
ya shilingi milioni mia moja si za kweli ni uongo mtupu.
Kwa mujibu wa Diwani Gwae baada
ya sala hiyo waathirika wa ajali hiyo kila moja amepewa shilingi
212,500 ikiwa ni rambarambi kwa kupoteza ndugu.Fedha hizo ni kutoka
fedha za ubani za shilingi 5 milioni zilizotolewa na mmiliki wa kampuni
ya summary na shilingi laki moja zilitolewa Mkuu wa mkoa wa Singida na
shilingi 150,000 zilizotolewa na wakazi wa kijiji cha Minyinga.
