Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu halmashauri ya jiji la Dar kuendesha operesheni safisha jiji katika maeneo mbalimbali ikiwemo Posta, na kuwaondoa wale wote wanaofanya biashara kwenye maeneo hayo hivi sasa wafanyabiahsra hao wamerejea kwa kasi
Hii leo mpigapicha wa Eddy Blog amepita Posta jijini humo na kushuhudia biashara zikiendelea kwa kasi ikiwemo za uuzaji wa magazeti na biashara nyinginezo ambazo askari wa jiji walivunjavunja meza za kuuzia magazeti wakati wa utekelezaji wa operesheni
Mara nyingi kumekuwa na utaratibu wa kuanzisha operesheni ambapo baada ya muda mfupi wafanyabiashara hao hurejea baada ya kuona ulegevu wa muendelezo wa mambo hayo
Habari/picha na Eddy Blog Team