Aliyekua Balozi wa
Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Ricky Mahalu
--
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA
Kuu Kanda ya Dar es Salaam,HIvi PUNDE imemfutia rufaa ya Kesi ya
uhujumu uchumi Na.1/2007 iliyokuwa ikimkabili Aliyekuwa Balozi wa
Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Ricky Mahalu na Grace Martin
Waliokuwa wakitetewa na Mawakili wa kujitegemea Beatis Malima, Mgongolwa,Cuthbert Tenga na Mabere Marando , iliyokuwa imekatwa na
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), dhidi ya Mahalu na Grace Kapinga hukumu
ya iliyotolewa na Aliyekuwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu Dar es Salaam ya Agosti 9 Mwaka 2012,Elvin Mugeta ambayo hukumu
hiyo iliwaachiria Huru wa jibu rufaa ambao walikuwa wakikabiliwa na Kesi
ya uhujumu Uchumi wa zaidi Ya Euro Milioni mbili Katika ununuzi wa Jengo
la Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.
Jaji
John Utamwa Alifikwa uamuzi wa kutoa amri ya Kuiondoa RUFAA hiyo
iliyokuwa imekatwa na DPP dhidi ya Mahalu na Grace kufuatia ombi
lililowasilishwa na DPP Mwenyewe lililokuwa likiomba Mahakama hiyo
iondoe RUFAA hiyo aliyokuwa ameikata dhidi ya wa jibu RUFAA hicho chini
ya Kifungu Cha 386(1) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka
2002 kwasababu DPP Hana Haja ya kuendelea na rufaa hiyo.