UMOJA wa Katiba ya Wananchi ( UKAWA ) umepokelwa kwa mabango yanayowapinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa yaliyokuwa yamebebwa na vijana....
Mabango hayo yalikuwa yanasomeka kuwa, "Tuna mashaka na ndoa ya UKAWA watauza nchi", huku yakisisitiza umuhimu wa vijana wa Wilaya ya Mufindi kutaka Serikali mbili.....
Pia mabango hayo yalikuwa yanawataka wajumbe wa UKAWA warudishe posho kwanza bungeni mjini Dodoma....
Katika
mkutano wao uliofanyika juzi mjini Mafinga Viwanja vya mashujaa,
mkutano huo uliendeshwa na mwenyekiti wa chama cha Wananchi (
CUF ) ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa UKAWA.....
Wengine
waliohutubia ni pamoja na mwakilishi wa chama cha
NNCR-Mageuzi,Danda Juju na kiongozi wa taasisi ya kiislam ya
Shura ya Imamu,Rajabu Katimba.....
Baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na vijana hao wilayani Mufindi yalikuwa na ujumbe uliosomeka: "Vijana Mafinga tuna mashaka na ndoa ya UKAWA,watauza nchi" na bango la waendesha bodaboda lilisomeka: "Rudisheni posho kwanza mjengoni Dodoma"
Mengine na ujumbe wake kwenye mabano ni lililowatambulisha wafanyabiashara wa sokoni lililosomeka, "Mafinga Sokoni,Serikali tatu siyo suluhisho la matatizo ya wananchi", na la wapiga debe mafinga stendi lilisomeka, "Karume Oyee, Nyerere Oyee, Muungano Saafi!".
Bango la waliojitambulisha kuwa ni machinga lilisomeka, "Tunataka Serikali inayojali wajasiriamali, siyo kujali matumbo yao"...Na lile la wakulima lilisomeka, "Kilimo Kwanza, Utaifa kwanza".
Wakati
mabango hayo yakizungushwa katika mkutano huo muda ambao
Profesa Lipumba alikuwa akihutubia, usikivu ulipotea kwa
takribani dakika 15 hadi 20 baada ya sehemu ya kundi la
vijana lililokuwa likimsikiliza kuelekea upande walikokuwa vijana
wenye mabango hayo....
Polisi
waliokuwepo walilazimika kuingilia kati kadhia hiyo na mzozo
huo baina yao na vijana waliokuwa na mabango ulisikika....
Mmoja wa polisi aliyekuwa akiwatuliza vjana hao alisema,"Jamani huu ni mkutano halali wa kisiasa, acheni wenzenu wafanye mkutano wao, yatoeni mabango yenu"
Mmoja wa vijana aliyekuwa amebeba bango mojawapo jina halikupatikana mara moja alisikika akisema, "UKAWA
siyo chama cha siasa, wao wanamtazamo wao na sisi tuna mtazamo
wetu, kwa hiyo siyo jambo la ajabu wakajua kwamba Mafinga
wengi hatuwaungi mkono na siyo dhambi kuonyesha hisia zetu
katika mkutano wao"
Akielezea
vurugu hizo, profesa Lipumba alisema zinafanywa na vijana
waliotumwa na CCM kwa sababu ya msimamo wao wa kutaka serikali
mbili, tuhuma zilizokanushwa na katibu wa CCM wilaya ya
Mufindi,Miraji Mtaturu aliyehojiwa baada ya mkutano huo...
"Siamini
kama mkutano huu ungekuwa unahutubiwa na mwenyekiti wa CCM wa
taifa Jakaya Kikwete wangekuja na mabango yao na kufanya
vurugu hizi," alisema Lipumba na sauti toka kwa baadhi ya vijana hao zikasikika zikisema, "Kama angekuja na msimamo wa serikali tatu ni lazima angekutana na mabango haya, sisi tunataka serikali mbili"
Hata baada ya vurugu hizo kutulia na Profesa Lipumba kuruhusu maswali baada ya kufafanua sababu mbalimbali zilizowafanya wasusie bunge la katiba na kuanzisha UKAWA, mkutano huo ulitaka kuvurugika tena....
Swali
liliotaka kuuvuruga mkutano huo lilitoka kwa kijana
aliyejitambulisha kwa jina la Rahid Rashid ambaye alitaka kujua
kwa nini CCM hawapo katika umoja huo.
Pamoja
na vijana wengine kupiga kelele wakiashiria kuwa hilo siyo
swali,Profesa Lipumba alijibu na kusema hilo ni swali zuri.
Alisema
milango ya UKAWA ipo wazi kwa mtu yeyote ndani na nje ya
bunge la katiba wakiwemo wabunge na viongozi wa CCM
"Tutafurahi
kuwapata wana CCM,tunawakaribisha UKAWA ili kwa pamoja
tushirikiane kupata katiba inayotokana na wananchi," alisema
Mwingine
aliyeuliza swali alikuwa Winfrida Ngoti aliyesema harakati za
kudai serikali tatu hazitakuwa na maana yoyote kama matatizo
ya wananchi hayatashughulikiwa.
"Watanzania
wana matatizo lukuki,vituo vya huduma za afya havina
wataalamu,dada,wakulima hawapati pembejeo kwa wakati na bei zake
ni kubwa, wafanyabiashara wadogo wanabanwa na kukamuliwa kodi,
walimu haapati mishahara kwa wakati, askari wana mishahara midogo
," alifafanua
Katika
majibu yake, profesa Lipumba alisema hayo yote yatafanyiwa kazi
kukiwa na katiba bora itakayosisitiza uwajibikaji na uadilifu.



