AFISA
Maendeleo ya jamii sekretariati ya mkoa wa Singida,Zuhura Kyaria
amesema mzee Abdi Nkambi lanjuu (75) aliyeishi wodini kwa zaidi ya miaka
45,ataendelea kubaki kwenye makazi yake hayo hayo ya wodini kwa madai
kwamba hana ndugu au mtu ye yote wa kuweza kumhudumia muda wote.
Akifafanua
Kyaria amesema kuwa baada ya juhudi kubwa kufanyika za kuwatafuta ndugu
zake kijijini kwao Mhintiri tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi kugonga
mwamba,walihamishia mawazo yao kumpeleka katika kambi ya watu wenye
ukoma ya Sukamahela wilayani Manyoni.
“Baada
ya kugonga mwamba huko Mhintiri,basi tupaona pengeni mahali
patakapomfaaa mzee Abdi kuishi,ni kwenye kambi ya wakoma ya
Sukamahela.Tulipomuuzia mzee Abdi wazo hilo,alikataa kuhamia
huko”,amesema.
Kyaria
amesema hata wao walipokaa chini na kutafakazi juu ya kumpeleka
Sukamahela,tulioona kwamba hapatamfaa kwa sasa anahitaji mtu wa
kumhudumia wakati wote,…yaani mchana na usiku kwa vile hawezi kukaa
kutokana na kupooza sehemu yake ya kuanzia kiunoni hadi chini kwenye
miguu.
“Kwa
haraka haraka tu,ukiangalia,pale kambi ya Sukamahela ina uhaba mkubwa
wa wafanyakazi,pia kuna uhaba wa maji na wakazi wenyewe wa sehemu
hiyo,ni watu ambao hawana vidole vya kujihudumia wenyewe,watawezaje
kuhudumia mtu mwingi ambayo sio ndugu yao”,amesema na kuongeza;
“Juzi
watu wa wazira ya afya na ustawi wa jamii waliposoma habari za mzee
Abdi kwenye gazeti la MWANANCHI,walinipigia simu na nikawaeleza ugumu wa
kumhamishia mzee Abdi katika kambi ya watu wa ukoma na wakanielewa”.
Afisa
huyo kwa ujumla mzee Abdi ataendelea kuwepo katika hospitali ya mkoa
mjini Singida,hadi hapo maisha yake ya duniani yatakapokoma.
Kwa
sasa mzee Abdi anachokiomba kwa jamii,serikali,asasi na watu wenye
uwezo,ni kumsaidia apate uhakika wa kupata huduma ya chakula kwa mujibu
wa mahitaji ya binadamu ye yote,ili aweze kuondokana na adha ya omba
omba ambayo inamwezesha kula mlo moja kwa siku.
