MTU MMOJA AFA KWA KUNYONGWA NA MAJAMBAZI MKOANI PWANI

Na John Gagarini, Kibaha 

MLINZI Bakari Mape (70) mkazi wa Mlandizi wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani ameuwawa kwa kunyongwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.

Watu hao ambao idadi yao haikuweza kufahamika mara moja walimwua mlinzi huyo kwa kumvunja shingo kisha kuiba kwenye duka ambalo mlinzi huyo alikuwa akililinda.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna Mwandamizi Msaidizi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa tukio  hilo lilitokea Mei 14 mwaka huu majira ya saa 8 usiku eneo la sokoni
Mlandizi wilayani hapa.


Kamanda Matei alisema kuwa watu hao baada ya kumwua marehemu ambaye alikuwa akilinda duka la Conrad Masawe (53) mkazi wa Mtongani Mlandizi, waliiba kiasi cha shilingi milioni 5.2.

"Walipomwua walingoa bati kisha kuingia ndani na kuiba fedha hizo na kutoweka kusikofahamika huku wakimwacha marehemu hapo," alisema Kamanda Matei.


Alisema kuwa kutokana na tukio hilo wanamshikilia mtu mmoja aitwaye
Omary Rajabu kuhusiana na suala hilo.





"Mwili wa marehemu ulikabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi baada ya
uchunguzi wa daktari na tutawasaka watu walihusika na tukio hilo ili
mkondo wa sheria uweze kuchukua hatua kwani kitendo hicho ni ukatili
ndani ya jamii," alisema Kamanda Matei.





Aidha aliwataka wafanyabiashara waajiri watu weny umri wa kati ili
waweze kukabiliana na matukio kama hayo na kuacha kuajiri watu wenye
umri mkubwa sana kwani ni vigumu kukabiliana na matukio kama hayo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo