MTOTO ACHOMWA MOTO NA BIBI YAKE BAADA YA KUIBA KARANGA ZA BIBI HUYO HUKO GEITA

Mwanafunzi wa darasa la tatu Sofia Damasi (12) wa shule ya msingi Lutozo katika kata ya Katoro wilayani Geita mkoani Geita amelazwa katika kituo cha afya mjini Katoro baada ya kuchomwa  moto sehemu mbalimbali za mwili wake na bibi yake.

Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 8 katika kitongoji cha Bulengahasi.

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa bibi huyo anayeitwa Monica Petro(50) ambaye ni mkazi wa Katoro aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya mjukuu wake huyo kumwibia karanga za mbegu alizokuwa amezitunza kwa ajili ya kupanda.

Akiongea kwa shida alikolazwa wodi ya wanawake mtoto huyo amesema kuwa alikumbwa na mkasa huo juzi majira ya saa 8 mchana muda mfupi baada ya kumaliza kula chakula cha mchana.

“Baada ya kumaliza kula chakula bibi yangu alitoka nikabaki mimi nyumbani na baba zangu wadogo wawili ambao nao baadaye waliondoka na kwenda kazini kwao na ndipo bibi yangu alirudi tena na kuingia jikoni’’,alieleza.

“Bibi alipoingia jikoni aliniita jikoni na nilipoenda jikoni bibi yangu alifunga mlango kwa ndani na kisha kunifunga kamba aina ya mpira mikononi mwangu na kuanza kunitesa’’alifafanua mtoto huyo/

Alisema mara baada ya kufanya unyama huo bibi yake alitoka nje na kumfungia ndani na ndipo alipoanza kupiga kelele za kuomba msaada ndipo majirani walifika na kumfungulia mlango na kamba hiyo na baada ya hapo walimpeleka kituo cha polisi na kupewa hati namba tatu ya matibabu(PF3) kwa ajili ya kupata matibabu na kisha kupelekwa kituo cha afya cha Katoro.


Afisa mtendaji wa kata ya katoroAloyce Kamuli alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema  hana taarifa kuhusu tukio hilo.

Na Valence Roberet Geita.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo